• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Masumbwi-Uganda, Bondia Sharif Bogere aweka rekodi ya kuwapiga mabondia wa Mexico.

  (GMT+08:00) 2018-01-29 09:31:08

  Bondia Sharif Bogere wa Uganda amemshinda kwa pointi Arturo Santos Reyes katika pambano la masumbwi la raundi kumi lililofanyika mjini Las Vegas, Marekani.

  Katika pambano hilo lililoandaliwa na kampuni ya Mayweather Promotions, Bogere alivuna alama nyingi katika raundi ya tano na saba ambazo zilimfanya awe na jumla kuu inayozidi ile ya Reyes.

  Huu ni ushindi wa 14 dhidi ya mabondia kutoka Mexico aliyowahi kupigana nao tangu Bogere aingie katika ulimwengu wa masumbwi.

  Katika pambano jingine lililofanyika siku hiyo hiyo, bondia mwingine kutoka Uganda Kennedy Katende alimshinda Lyubomyr Pinchuck wa Ukraine katika pambano lililofanyika mjini Philadelphia nchini Marekani.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako