• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tennis, Ushindi wa Federer katika fainali ya Australia waandika rekodi mpya nyingi.

    (GMT+08:00) 2018-01-29 09:39:50

    Roger Federer wa Uswisi amefanikiwa kutetea taji lake la ubingwa wa mashindano ya tennis ya Australia kufuatia ushindi aliopata jana kwenye mechi ya fainali alipocheza dhidi ya Marin Cilic wa Croatia.

    Federer alimshinda Cilic kwa seti 6-2 7-6 6-3 3-6 na 6-1, na kumfanya sasa ashinde ubingwa wa Australia kwa mara ya sita rekodi ambayo ni sawa na Novak Djokovic wa Serbia na Mzee Roy Emerson wa Australia.

    Lakini kwa upande wa wachezaji wanaume, Federer anaweka rekodi ya kushinda mataji mengi ya michuano mikubwa akifikisha 20, rekodi ambayo duniani ni wanawake watatu tu, ndiyo wamewahi kufikisha, Serena Williams wa Marekani 23, Steffi Graf wa Ujerumani 22 na Margareth Court wa Australia 24.

    Kwenye michuano ya Australia mwaka huu taji hilo limekwenda kwa Caroline Wozniacki wa Denmark aliyemshinda Simona Halep wa Romania katika mechi ya fainali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako