• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Uzinduzi wa maonyesho ya Kimataifa ya Zao Kahawa-Pu'er Yunnan

  (GMT+08:00) 2018-01-30 10:20:48

  Viongozi kutoka nchi mbalimbali wakiongozwa na Kansela wa ubalozi wa Ethiopia nchini China Getachew Uta leo wamehudhuria uzinduzi wa maonyesho ya kimataifa ya zao la kahawa ya Pu'er.

  Mji wa Pu'er uliopo katika mkoa wa Yunnan kusini mwa China, na unasifika zaidi kwa kilimo cha kahawa yenye ubora na halisi.

  Kando ya hafla hiyo ya uzinduzi naimebahatika kuzungumza na kansela Uta, ambaye amenieleza namna ambavya Afrika inaweza kunufaika kwa kutokana na ushirikiano wa kibiashara na China, kwa kujifunza uzoefu wa uzalishaji bora na kupata kupanua soko la kahawa kutoka Afrika.

  Bw. Uta anasema, "Nimeshangazwa sana, kwani nafahamu kuwa waChina hupendelea sana kunywa chai, lakini kumbe wamewekeza pia katika uzalishaji kahawa, mfano mzuri ni kwenye maonyesho ya kimataifa ya kahawa, unashuhudia jinsi wanavyoendelea vizuri. Uzalishaji bora ni jambo ambalo wazalishaji wa Afrika wanaweza kujifunza kutoka China, lakini soko liko kote duniani, pia kutokana na jamii ya China kuanza kutumia kahawa hiyo pia ni faida kwa nchi za Afrika."

  Kahawa ya Pu'er ni aina ya Arabica yenye ladha ya kipekee ambayo inasifika dunia nzima kwa kiwango chake cha juu cha ubora.

  Wageni toka nchi mbalimbali hufika si tu kuonja utamu wa kahawa hii bali huvutiwa na utamaduni wa watu wa mji huo pamoja na vivutio vya utalii vilivyo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako