• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Soka, Tetesi za Usajili: Arsenal wakubali kulipa pauni milioni 60 kwa ajili ya Aubameyang

    (GMT+08:00) 2018-01-30 10:55:33

    Mchezaji wa kimataifa wa Brazil, Lucas Moura amewasili jijini London kwa ajili ya zoezi la kufanya vipimo vya afya kwa ajili ya kujiunga na klabu ya Tottenham akitokea klabu ya PSG ya nchini Ufaransa.

    Ada ya uhamisho wake imetajwa kuwa pauni milioni 25 ikiwa ni ushauri uliotolewa na kocha wa Tottenham kwamba yafaa timu kuimarishwa zaidi ili kufanya vizuri katika msimu wa ligi na ligi ya klabu bingwa.

    Tangu ajiunge na PSG mwaka 2013 Moura amecheza mechi 150 akifanikiwa kutwaa vikombe vingi vya ubingwa ikiwemo vine vya ligi kuu ya Ufaransa.

    Kwingineko Mchezaji wa Liverpool Daniel Sturridge amejiunga na klabu ya Westbrom Albion kwa mkopo katika kipindi chote cha msimu kilichosalia.

    Taarifa nyingine kutoka London zinasema kuwa Klabu ya Arsenal imekubali kutoa pauni milioni 60 kwa ajili ya kumchukua Pierre Emerick Aubameyang kutoka klabu ya Borussia Dortmund.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako