• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Kampuni ya kujenga barabara ya Ngong mjini Nairobi

    (GMT+08:00) 2018-01-30 19:34:51

    Kampuni moja ya Japan imepewa kandarasi ya kutekeleza mradi wa awamu ya pili ya ujnezi wa barabara ya Ngong mjini Nairobi kutoka eneo la Prestige Plaza kwenda Dagoretti Corner.

    Mkuu wa mamlaka ya barabara za mijini Silas Kinoti amesema ujenzi wa barabara hiyo utaanza mwezi machi.

    Mradi huo wa kilomita 2.42 utagharimu shilingi bilioni 2.3.

    Kampuni hiyo ya World Kogyo Kaihatsu (WKK) imesema itatekeleza mradi huo wa laini mbili za barabara ndani ya miaka miwili.

    WKK pia ndio ilitekeleza mradi wa kujenga barabara kati ya maktaba ya kitaifa na Prestige Plaza kwa gharama shilingi 1.4.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako