• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda: Sekta ya kibnafsi Uganda yataka kupunguziwa ushuru

    (GMT+08:00) 2018-01-30 19:35:52

    Viongozi wa wakfu wa sekta ya kibinafsi nchini Uganda wameitaka serikali kupunguza ushuru kwa sekta hiyo.

    Mwenyekiti wa halmashauri ya wakfu huo Patrick Bitature amesema serikali inatoza ushuru mkubwa kwa sekta hiyo na hivyo kuathiri shughuli zao za kibiashara.

    Alisema serikali badala yake inafaa kupanga upya ukusanyaji wake wa ushuru ili kuhakikisha kila mtu anachangia.

    Katika bajeti ya mwaka 2018/19 serikali itahitaji karibu shilingi trilioni 30 huku mamlaka ya ushuru nchini humo URA ikitarajiwa kukusanya nusu ya fedha hizo.

    Waziri mkuu wa Uganda, Ruhukana Rugunda amesema anafahamu uzito wa ushuru wa juu unaotozwa sekta ya kibinafsi na kuahidi kuwa serikali itaongeza uwezo wake wa kukusanya kodi ili kulinda wafanyabiadhara.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako