• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Wafugaji wa ng'ombe Kinondoni walalamikia kukosa soko

    (GMT+08:00) 2018-01-30 19:36:15

    Wafugaji wa ng'ombe wa maziwa wilayani Kinondoni nchini Tanzania wamelalamikia maziwa kukosa soko hali inayosababisha wayamwage.

    Walitoa kilio hicho mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi wakati wa uzinduzi wa Mtando wa Wafugaji wa Ng'ombe wa Maziwa.

    Katibu wa mtandao huo, Faustine Mbassa alisema kuna changamoto ya kuwapata wateja wanaohitaji maziwa.

    Alifafanua kuwa wameamua kuanzisha mtandao huo ili wawe na umoja wa kutafuta masoko ya maziwa.

    Hata hivyo, Takwimu za Bodi ya Maziwa Tanzania (TDB) zinaonyesha kuwa unywaji wa maziwa nchini ni wastani wa lita 47 kwa mtu mmoja kwa mwaka wakati Shirika la Chakula Duniani (Fao) linapendekeza kunywa lita 200.

    Nchini Kenya, unywaji wa maziwa ni wastani wa lita 120 kwa mtu mmoja kwa mwaka wakati Uganda ni lita 50 kwa mtu mmoja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako