• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Waziri aagiza viwanda vya samaki kufunguliwa

    (GMT+08:00) 2018-01-30 19:37:01

    Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina ameagiza viwanda vinne vya kuchakata minofu ya samaki vilivyofungwa vya Tan Perch Limited, Supreme Perch Limited, Mara Fish Packers Limited na Prime Catch Limited kufunguliwa ifi kapo Julai Mosi mwaka huu.

    Pia Waziri Mpina ameagiza wamiliki wa viwanda hivyo vilivyofungwa vilivyoko katika mikoa ya Mwanza na Mara kuwasilisha Wizara ya Mifugo na Uvuvi mpango kazi wa namna ya kuvifufua kabla ya kufikia mwezi Machi huu.

    Akizungumza kwa nyakati tofauti na maelfu ya Wavuvi katika Mwalo wa Bwai Kumsoma, Rorya na Mwalo wa Kisorya, Bunda, Mara, Waziri alisema hadi kufikia Juni mwaka huu samaki watakuwa wa kutosha Ziwa Victoria.

    Pia Waziri Mpina alishiriki zoezi la kuteketeza zana haramu za uvuvi zenye thamani ya Sh bilioni 3.2 zilizokamatwa na kikosi cha kupambana na kudhibiti uvuvi haramu na utoroshaji wa mazao ya uvuvi Kanda ya Mara.

    Alisisitiza msimamo wa Serikali ya awamu ya tano wa kuendelea kupambana na uvuvi haramu hadi pale utakapokoma katika Ziwa Victoria.

    Alisema operesheni hiyo maalumu ya kupambana na uvuvi haramu inayoendelea katika Ziwa Victoria haitakuwa na

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako