• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Usain Bolt, Afanya mazoezi ya kandanda na mabingwa wa soka Afrika, Mamelodi Sundowns nchini Afrika Kusini

    (GMT+08:00) 2018-01-31 10:50:09

    Binadamu mwenye kasi zaidi duniani, raia wa Jamaica Usain Bolt, alijiunga na klabu ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini kwa mazoezi katika uwanja wao wa mazoezi wa Chloorkop jana jumatatu.

    Mabingwa hao wa soka Afrika wa mwaka 2016 walitangaza kuwasili kwa Bolt kupitia Twitter na kupakia video ya Mjamaica huyo akifanya mazoezi na wachezaji.

    Bolt amealikwa kufanya mazoezi wiki moja na klabu ya Ujerumani ya Borussia Dortmund mwezi Machi na anapanga kukubali mwaliko huo.

    Bolt alistaafu riadha Agosti mwaka jana baada ya mashindano ya ubingwa wa dunia jijini London mara nyingi amekuwa akionyesha nia ya kujiunga na kandanda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako