• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Masumbwi, Bondia Khan amrushia chupa ya maji mpinzani wake kwenye mkutano na waandishi wa habari

    (GMT+08:00) 2018-01-31 10:51:14

    Wakati wa mkutano na waandishi wa habari jana Bondia Amir Khan wa Uingereza alimrushia maji, mpinzani wake katika pambano lake la April 21, Phil Lo Greco wa Canada.

    Khan alidai kuwa amelazimika kufanya hivyo baada ya madai kuwa mpinzani wake huyo anaacha kuzungumzia zaidi udhaifu wa kimichezo, anakwenda mbali zaidi kuzungumza masuala binafsi yakiwemo ya kifamilia.

    Baada ya watu wa usalama kurejesha utulivu, Promota wa pambano lao hilo, Eddie Hearn alimwamuru Greco kuomba radhi kwa Khan.

    Lakini Khan aliwaomba radhi walioshuhudia tukio hilo na akisema tabia ya mpinzani wake huyo inamuongeza hasira ya kumshinda April 21 watakapopanda ulingoni mjini Liverpool.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako