• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya-Wafanyabiashara walifunga biashara zao jana wakihofia ghasia

    (GMT+08:00) 2018-01-31 19:05:14

    Wafanyabiashara wengi jijini Nairobi jana waliandikisha hasara kutokana na hofu labda kungezuka ghasia wakati wa shughuli ya kuapishwa kwa kiongozi wa upinzani Raila Odinga.

    Barabara za katikati mwa jiji zilikuwa na magari machache huku mengi ya magri yanayosafirisha abiria vijijini hayakufanya kazi.

    Madereva wa safari za mbali walilalamika kukosa biashara kutokana na shughuli iliyokuwa katika bustani ya Uhuru Park.

    Pia wachuuzi wanaoonekana katikati mwa jiji pia hawakuwa wengi jana kama siku za kawaida.

    Wafanyabiashara wengi walihofia kupata hasara kwani walihofia kungekuwa na machafuko katikati mwa jiji,hata hivyo hakukuwa na visa vyovyote vya machafuko au ghasia.

    Hali ya kawaida inatarajiwa kurejea leo.Maduka mengi yamefungua biashara katikati mwa jiji na wachuuzi pia wameanza kufurika jijini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako