• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania-Dk Mengi atoa fursa kwa Chama cha Wafanyabisahara Wanawake Tanzania (TWCC)

    (GMT+08:00) 2018-01-31 19:05:43

    Mwenyekiti wa sekta binafsi Tanzania (TPSF) ,Dk Reginald Mengi amekipatia Chama cha Wafanyabiashara Wanawake Tanzania (TWCC) jingo la IPP lililopa katika viwanja vya Sabasaba ili watumie kutangaza bidhaa zao.

    Pia amewapa nafasi ya kutangaza bure fursa za TWCC kwenye gazeti la Nipashe kwa mwaka mzima na chama hicho kitatakiwa kuyatengeneza matangazo yao ambayo yataingizwa ndani ya gazeti.

    Dk Mengi alitoa ahadi hiyo jana jijini Dar es Salaam wakati akifungua mkutano mkuu wa mwaka wa TWCC,uliohudhuriwa na wanachama kutoka mikoa mbalimbali.

    Dk Mengi alisema katika kuunga mkono juhudi zao,ameridhia ombi lao la kulitka jingo hilo la IPP walitumia kutangaza bidhaa zao kimataifa wakati wa maonyesho ya Sabasaba.

    Ombi hilo lilitolewa mwaka jana na Mwenyekiti wa Taifa wa TWCC,Jacqueline Maleko wakati wa maonyesho ya Sabasaba na kulirudia tena jana kwenye mkutano huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako