• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya-Makampuni ya China yashinda zabuni ya ujenzi wa nyaya za umeme wenye gharama ya Sh9.6bn katika kaunti ya Turkana

    (GMT+08:00) 2018-01-31 19:06:04

    Makampuni ya China yamepewa zabuni ya ujenzi wa nyaya za kusambaza umeme utakaounganisha mradi wa nishati ya upepo ya Ziwa Turkana hadi kwa gridi ya taifa kufikia tarehe 31 Agosti kufuatia kukatizwa kwa mkataba wa kampuni ya Uhispania mwaka jana.

    Mkampuni ya NARI Group Corporation na Power China Guizhou Engineering Company, wameeleza nia yao ya kulipa faini Sh1.3 billion (€10 million) kila mwezi iwapo yatashindwa kufikia makataa ya tarehe 31 Agosti.

    Kulingana na kampuni ya usambazaji umeme ya Kenya Electricity Transmission Company (Ketraco),ambayo jumanne ilitia saini mkataba na kampuni za China,ujenzi huo wa nyaya za umeme wenye urefu wa kilomita 428 sasa hivi umefikia asilimia 70.

    Ujenzi wa mradi huu ulikwama kutokana na kukatizwa kwa mkataba wa kampuni ya Hispania ya Isolux mwezi Agosti mwaka jana baada ya kampuni hiyo kuwekwa chini ya urasimu kutokana na madeni.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako