• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Soka, Kenya: CAF wamaliza utata kuhusu matangazo ya mechi za AFC na Gor katika michuano ya Afrika mwezi ujao.

    (GMT+08:00) 2018-02-01 14:39:14

    Shirikisho la Mpira wa Miguu barani Afrika CAF, limetangaza mabadiliko ya tarehe ya mechi ya awali ya mchujo wa kombe la Shirikisho kwa vilabu, kati ya AFC Leopards ya Kenya na Fosa Juniors ya Madagascar.

    Badala ya kufanyika Februari 10 sasa utachezwa Februari 11, lengo likiwa ni kuupishanisha na mchezo mwingine utakaopigwa Februari 10, wa klabu bingwa Afrika kati ya Gor Mahia na Leones Vegetarions ya Equatorial Guinea.

    Lakini uwanja utakaotumika uanabaki kuwa ule ule wa Bukhungu wa mjini Kakamega, jambo la msingi pia ikiwa ni kutoa fursa ya matangazo ya moja kwa moja kugawanyika kwa ufasaha pasi na kuingiliana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako