• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Soka, Uganda: Mashabiki wa Express FC watakiwa kuacha lawama, waunge mkono juhudi za kuinusuru isishuke daraja.

    (GMT+08:00) 2018-02-01 14:39:39

    Kuelekea mzunguko wa pili wa ligi kuu nchini Uganda, mabingwa wa zamani Express FC wamefanikiwa kufanya usajili wa wachezaji sita ili kuziba upungufu uliokuwepo katika mzunguko wa kwanza.

    Wachezaji walioongezwa katika kikosi hicho ni Mabeki watatu, Ayub Kisalita, Alfred Leku na Joseph Ssemujju, wengine ni Isaac Kisujju, Jalil Zimula na Shafik Kakeeto.

    Mwenyekiti wa klabu hiyo ambayo kwa sasa ni ya pili kutoka chini katika msimamo wa ligi hiyo yenye timu 16, Bi. Florence Nakiwala amewataka mashabiki kuacha kulaumu na wawe watulivu wakati suala la kuinusuru timu hiyo isishuke daraja linashughulikiwa kitaalam.

    Katika hatua nyingine klabu hiyo imelipa mishahara ya wachezaji na kocha mkuu ikiwa ni mapema, jambo alilosema ni kuwaondolea mawazo ya fedha.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako