• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Soka, Matokeo ya Ligi Kuu Uingereza: Chelsea na Manchester United zakumbana na vipigo

    (GMT+08:00) 2018-02-01 14:40:51

    Tottenham Hotspurs jana imejongezea kasi ya kusaka nafasi ya kuingia nne bora katika msimamo wa ligi kuu soka nchini Uingereza baada ya kuifunga Manchester United kwa magoli 2-0 mjini London.

    Magoli ya Spurs yalifungwa katika kipindi cha kwanza Christian Erickssen katika sekunde ya 11, na goli la pili likipatikana baada ya Jone kujifunga katika dakika ya 28.

    Chelsea wameshuka kwa nafasi moja kwenye msimamo baada ya kukubali kipigo cha magoli 3-0 jana wakiwa nyumbani kutoka kwa AFC Bournemouth.

    Lakini Manchester City wamefanikiwa kurejesha tofauti ya pointi na timu ya pili kwenye msimamo ambapo sasa ni 15, baada ya ushindi wa magoli 3-0 iliopata jana dhidi ya West Brom Albion.

    Ligi hiyo inaendelea tena jumamosi Februari tatu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako