• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Soka, Uhamisho wa wachezaji uliofanyika katika siku ya mwisho ya usajili.

  (GMT+08:00) 2018-02-01 14:44:45

   Kama ilivyotabiriwa, Historia imeandikwa katika siku ya kufungwa kwa dirisha dogo la usajili barani ulaya jana, baada ya timu tatu za Arsenal, Borussia Dortmund na Chelsea kufanya mzunguko wa pembe tatu katika usajili (Transfer Triangle), ambapo kila timu ilitoa na kupokea katika zenyewe.

  Arsenal ilimchukua Pierre Aubameyang wa Dortmund na kumtoa Olivier Giroud ambaye alikwenda Chelsea kumtoa Michy Butshuayi aliyelazimika kwenda kwa mkopo Dortmund ambako atasaidia kuziba pengo lililoachwa Aubameyang.

  Mzunguko huu umechambuliwa na wajuzi wa masuala ya soka, kuhusu manufaa na mapungufu kwa katika timu walizokwenda ama wanakotoka wachezaji hao.

  Katika hamisho zingine za mwisho mwisho jana, Islam Slimani wa Algeria amekwenda Newcastle kwa mkopo akitokea Leceister City, na Swansea ilikamilisha sakata la kumrejesha Andey Ayew aliyeondoka klabuni hapo mwaka 2016 na kutimkia West Ham.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako