• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mauzo ya rejareja ya bidhaa za matumizi nchini China yaongezeka kwa asilimia zaidi ya 10 kwa miaka 14 mfululizo

    (GMT+08:00) 2018-02-01 17:22:33

    Thamani ya jumla ya mauzo ya rejareja ya bidhaa za matumizi nchini kwa mwaka 2017 ilifikia dola za kimarekani trilioni 5.8, na kuongezeka kwa asilimia 10.2 kuliko mwaka jana, ambalo ni ongezeko la zaidi ya asilimia 10 kwa miaka 14 mfululizo.

    Kwa mujibu wa Wizara ya Biashara ya China, mauzo ya rejareja yamekuwa injini kubwa katika kukuza uchumi wa China kwa miaka minne mfululizo. Pia mwaka jana watu waliojikita kwenye sekta ya biashara ya ndani walifikia milioni 192, idadi ambayo iliongezeka kwa asilimia 10 kuliko mwaka juzi na kuchukua karibu robo moja ya wafanyakazi wote nchini humo.

    Takwimu pia zinaonesha kuwa, mwaka jana mauzo ya rejareja katika mtandao wa internet nchini China yaliendelea kuongezeka kwa kasi kwa kuzidi makadirio ya soko.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako