• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya:Utata wa bilioni 35 za kandarasi za miundo msingi

    (GMT+08:00) 2018-02-01 20:02:49

    Utata wa billioni 35 wa fedha wanayodaiwa na serikali za kaunti na wanakandarasi huenda zikatatiza utendakazi wa serikali za kaunti.

    Baraza la magavana limesema seriali za kaunti zinadaiwa mabilioni ya pesa na wanakandarasi kwa sababu seriali kuu imechelewa kutoa pesa kwa serikali za kaunti hizo.

    Wanakandarasi wanasemekana wanadai serikali za kaunty takriban shilling billiioni 35.84 za kufikia mwezi Juni mwaka uliopita. Baraza hilo linasema kati ya mwezi Julai na Disemba mwaka uliopita, hazina kuu imetoa kwa serikali za kaunti pesa za kulipia mishahara ya wafanyikazi pekee na za kugharamia shughuli za serikali za kaunti hizo kwa sababu ya kubadilishwa kwa uongozi wa kaunti na kucheleweshwa kwa utekelezaji wa sheria ya ugavi wa raslimali za kaunti.

    Kulingana na kumbukumbu, serikali za kaunti zilipokea mgao wao wa kwanza wa pesa tarehe kumi na tisa mwezi huu. Baraza hilo limesema serikali za kaunti mwanzo zitazingatia ulipaji wa madeni yao. Kwa mfano seriali ya kaunti ya Mombasa inadaiwa deni la jumla ya shilling billion 3.95 Turkana shilling billion 2.9, Nakuru shilingi bilioni 2.8 na Kisumu shilling billion 1.8.

    Ni kaunti ya Kitui pekee ambayo haikuwa ikidaiwa deni lolote hadi mwezi Juni mwaka uliopita.

    kaunti ya Nairobi inadzaiwa na wenakandarasi takriban shilling billion 60 kulingana na kesi iliyowasilishwa katika mahakama ya millimani ambapo gavana Mike Sonko anaitaka mahakama kuu kusimamisha ulipaji wa pesa hizo hadi malipo wanayodai wanakandarasi yachunguzwe.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako