• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mahakama ya Usuluhishi Michezoni, yafuta vifungo vya maisha kwa wachezaji wa Urusi

    (GMT+08:00) 2018-02-02 10:19:55

    Mahakama kimataifa ya Usuluhishi wa masuala ya michezo CAS, jana imefuta adhabu za kufungiwa maisha na kutoruhusiwa kushiriki mashindano kwa wanamichezo 28 kutoka Urusi, kutokana na kile kilichodaiwa kuwa ni ushahidi wa wao kuwa na hatia kutojitosheleza.

    Wanamichezo wengine 11 waliofungiwa kesi zao bado zinaendelea kujadiliwa.

    Lakini pamoja na kufunguliwa vifungo vyao, wachezaji hao hawataweza kushiriki mashindano ya majira ya baridi yanayoanza Februari 9 nchini Korea Kusini kwani muda wa usajili umekwisha, licha ya kuwa wengi wao ni mabingwa watetezi katika baadhi ya michezo.

    Kwa upande wake, Kamati ya kimataifa ya Olimpiki imesema, jambo hilo litaathiri vita dhidi ya matumizi ya dawa za kuongeza nguvu michezoni, na kwa kuwa haijaridhika na uamuzi huo imepanga kukata rufaa katika mahakama ya juu zaidi nchini Uswisi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako