• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Pilika za safari katika kipindi cha sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa kichina zaanza rasmi nchini China

    (GMT+08:00) 2018-02-02 18:36:01

    Pilikapilika za kusafiri katika kipindi cha sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa kichina zimeanza rasmi kwa mwaka huu nchini China.

    Kwa mujibu wa kampuni ya reli ya China, idadi ya watu wanaotarajiwa kusafiri kwa treni kipindi hicho kitakachodumu kwa siku 40 itafikia milioni 390. Safari 428 za treni zimeongezwa katika kipindi hicho kutoka safari 7,638 za kila siku, na kuweza kuwasafirisha abiria milioni 8.14 kwa siku.

    Ili kukabiliana na uwezekano wa kutokea hali mbaya zaidi ya hewa, idara za treni zimekamilisha mipango ya dharura, kufanya matayarisho ya kutosha na kushikilia msimamo wa "maisha kwanza, usalama kwanza" ili kuhakikisha pilikapilika hizo zitaendelea vizuri.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako