• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania yateketeza vipodozi vya thamani ya shilingi bilioni 1.36

    (GMT+08:00) 2018-02-02 19:52:59

    Serikali ya Tanzania imesema jumla ya tani 407.82 za vipodozi vilivyopigwa marufuku vyenye thamani ya Sh bilioni 1.36 ziiliteketezwa na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) na kesi 52 zimefunguliwa baada ya upelelezi kukamilika.

    Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Faustine Ndugulile amesema katika mwaka wa fedha 2016/2017, TFDA ilitenga na kutumia Sh milioni 154.8 kwa ajili ya operesheni ya bidhaa vikiwemo vipodozi. Kwa mujibu wa Ndugulile, katika mwaka huu wa fedha , 2017/2018, mamlaka hiyo imetenga Sh milioni 132.2 ambazo zimekuwa zikitumika katika operesheni za kubaini na kukamata vipodozi haramu.

    Kauli hiyo inakuja muda mfupi tu baada ya bunge la Tanzania kutaka kujua mipango ya serikali katika kudhibiti vipodozi visivyo na viwango pamoja na gharama serikali inazoingia katika udhibiti wa bidhaa hizo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako