• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali za kaunti zatakiwa kubuni vivutio vya utalii

    (GMT+08:00) 2018-02-02 19:53:16

    Waziri wa Utalii na wanyamapori Najib Balala amezitaka kaunti zote kubuni vivutio vya pekee kwa lengo la kuimarisha utalii katika maeneo hayo.Balala amesema lazima mikakati mipya ibuniwe kwa lengo la kuongeza idadi ya watalii wa kimataifa na wa humu nchini.Ameongeza kuwa licha ya kuwa utalii kuwa na uwezo mkubwa wa kuiletea Kenya mapato mengi, idadi ya watalii bado ni chini sana ikilinganishwa na mataifa mengine ulimwenguni.Ripoti inasema hadi kufikia sasa ni watalii milioni moja tu ambao huweza kufika nchini Kenya kwa mwaka mmoja.Waziri amesema ilikuwa jambo muhimu kukumbatia utalii wa humu nchini kwa sababu ni sehemu muhimu sana ya kuendeleza shughuli za kitalii hasa wakati utalii wa kimataifa unapoenda chini.Amesisitiza kuwa kuna haja kubwa ya maeneo ya kaunti kujijrnga kitalii ili kuwa na umaarufu katika aina za kipekee za utalii.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako