• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yaonya kuhusu uwezekano wa kupanda kwa gharama za maisha

    (GMT+08:00) 2018-02-02 19:54:06

    Serikali ya Kenya imeonya kuwa huenda gharama ya maisha ikapanda kutokana na kupanda kwa bei ya mafuta.Waziri wa Kawi Bw Charles Keter amesema hali hiyo inachangiwa na kuendelea kupanda kwa bei ya mafuta ghafi katika masoko ya kimataifa tangu octoba mwaka jana.Hivi sasa bei hiyo imepanda kutoka dola 30 mwezi Octoba hadi dola 60 Disemba mwaka 2017.Keter amesema ni kutokana na hali hiyo ambapo mwezi huu tume ya kudhibiti sekta ya kawi ERC iliongeza bei ya petroli kwa shilingi 2.13 na 2.39. Kulingana na mpangilio wa bei uliotangazwa Januari 14 mafuta aina ya super petroli itauzwa shilingi 103 mjini Mombasa, 106 mjini Nairobi na shilingi 108 katika miji ya Kisumu na Eldoret. Nayo Dizeli itauzwa kwa shilingi 91.5 mjini Mombasa, shilingi 94 mjini Nairobi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako