• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Januari 29-Februari 2)

    (GMT+08:00) 2018-02-02 20:05:30

    Marekani yawapa wakimbizi wa Syria ruhusa kuishi nchini humo

    Serikali ya Marekani imeongeza kinga ya muda kwa karibu wakimbizi 7,000 wa Syria wanaoishi nchini humo wakati vita vikiendelea nchini mwao.

    Walikuwa wamepewa kinga ya muda dhidi ya ya kurejeshwa nyumbani chini ya mpango wa kibinadamu unaofahamika kama -Temporary Protected Status (TPS).

    Rais Trump amefuta mpango huo kwa nchi mbali mbali katika kipindi cha miezi ya hivi karibuni, na hivyo kuwaathiri wahamiaji kutoka kutoka El Salvador, Haiti na Nicaragua.

    Marekani ilikuwa imesema kuwa haitakubali maombi ya wahamiaji kupitia TPS kutoka Syria.

    Mpango wa hadhi ya ulinzi kwa raia wa Syria ulipangwa kufikia kikomo tarehe 31 Machi.

    Mapema mwaka huu, Wizara ya Usalama wa Ndani ilitangaza kuwa itafikisha kikomo mpango wa kinga kwa raia 262,500 kutoka El Salvador, ingawa hatua hiyo itacheleweshwa kwa miezi 18.

    Mwezi Novemba, utawala huo ulisema kuwa hadhi ya ukimbizi ya raia takriban 59,000 wa Haiti itakwisha 2019.

    1  2  3  4  5  6  7  8  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako