• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China inapinga kithabiti Mapitio ya Hali ya Nyuklia ya Marekani

    (GMT+08:00) 2018-02-04 16:19:41

    China imepinga kithabiti Mapitio ya Hali ya Nyuklia NPR yaliyotolewa na Wizara ya Ulinzi ya Marekani.

    Msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya China Ren Guoqiang amesema ripoti hiyo ya Marekani inayoichukulia China kama ni "changamoto kuu dhidi ya maslahi ya Marekani barani Asia imepotosha madhumuni ya maendeleo ya China na kutia chumvi tishio la nguvu ya nyuklia ya China.

    Ren amesisitiza kuwa China inashikilia kithabiti maendeleo ya kiamani na kuhimiza kuwa sera ya ulinzi wa kitaifa ni yenye asili ya kujilinda. China pia inafuata sera ya kutokuwa kwanza ya kutumia silaha za nyuklia wakati wowote na hali yoyote, kutotumia na kutishia kutumia silaha za nyuklia katika hali yoyote dhidi ya mataifa yasiyo na silaha za nyuklia au maeneo yasiyo na silaha ya nyuklia.

    Ameongeza kuwa China imejizuia kadri iwezavyo katika kuendeleza silaha za nyuklia na kuweka ukomo kwa uwezo wake wa nyuklia hadi kukidhi mahitaji ya kimsingi ya usalama wa kitaifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako