• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • mashindano ya dunia: Ujerumani yafuzu robo fainali kwa kuifunga Australia

    (GMT+08:00) 2018-02-05 08:44:17

    Alexander Zverev wa Ujerumani jana amemshinda Nick Kyrgios wa Australia na kulifanya taifa lake kufuzu kwenda hatua ya robo fainali ya mashindano ya kimataifa ya Tennis (Davis Cup)

    Zverev alishinda kwa seti yenye alama 6-2 7-6 na 6-2, na sasa timu yake itakutana na Hispania katika mechi ya robo fainali.

    Timu zingine zilizofuzu robo fainali ni Italia iliyoifunga Japan, Croatia kwa kuifunga Canada na Ubeligiji iliyoifunga Hungary.

    Nao mabingwa watetezi wa michuano hiyo, Ufaransa walifanikiwa kufuzu robo fainali kwa mara ya tisa mfululizo baada ya kuifunga Uholanzi, na Hispania wamefuzu kwa kuifunga timu ya Uingereza.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako