• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ofisa wa China asisitiza utekelezaji wa mkakati wa kustawisha vijiji unahitaji uwekezaji halisi

    (GMT+08:00) 2018-02-05 12:12:05

    Mkurugenzi wa ofisi ya kikundi cha uongozi wa kazi ya vijiji cha serikali kuu ya China Bw. Han Jun hapa Beijing amesema, mkakati wa kustawisha vijiji ni mkakati mkubwa wa chama na taifa, ambao pia ni jukumu la kihistoria litakalodumu kwa muda mrefu. Pia amesisitiza kuwa mkakati huo unazingatia sana utekelezaji, ambao unahitaji uwekezaji halisi na mazingira bora yenye sera kamili zaidi.

    Ofisi ya habari ya baraza la serikali la China limetoa waraka wa kwanza wa mwaka 2018 unaoelekeza utekelezaji wa mkakati wa kustawisha maeneo ya vijijini. Waraka huo umeeleza mustakabali wa sera za kuharakisha utandawazi wa kisasa wa kilimo na vijiji na kuchukua njia ya kustawisha vijiji ya usoshalisti wenye sifa ya kichina.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako