• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Timu zinazoshika nafasi ya juu kwenye msimamo wa ligi kuu maalum zaanza kwa ushindi raundi ya pili

  (GMT+08:00) 2018-02-06 09:04:48

  Timu wababe katika ligi maalum ya mchezo wa raga nchini Uganda, zimeanza kwa kasi raundi ya pili msimu huu kwa kupata ushindi kwenye mechi zao za kwanza.

  Timu hizo ni Buzz Pirates ambao ni vinara wa ligi hiyo walioifunga impis kwa alama 31-3 na Betway Kobs wanaoshika nafasi ya pili wakiwashinda Rams jambo ambalo lilipunguza tofauti ya pointi dhidi ya vinara.

  Rimula Rhinos wako nafasi ya tatu, katika mechi yao iliyopigwa mwishoni mwa juma lililopita walijikuta wakifanya kazi ya ziada, kusawwazisha matokeo na kasha kuibuka na ushindi dhidi ya Warriors, lakini Hima Heathens ndiyo walitia fora kwa kupata matokeo ya 60-3 dhidi ya Hippos na kuendelea kukamata nafasi za juu katika ligi hiyo.

  Lakini macho na masikio ya mashabiki wa ligi hiyo maarufu kama Nile Special premiership itakuwa katika yatakuwa katika mechi kali kati ya vinara Buzz Pirates na Hima Heathens.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako