• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Chama cha riadha chatangaza ongezeko la timu katika mbio za nyika mwaka huu

    (GMT+08:00) 2018-02-06 09:06:17

    Shirika la hifadhi ya wanyama pori pamoja KWS na shirikisho la vijana nchini Kenya NYS ni taasisi ambazo zinatarajia kutoa timu kwa ajili ya mashindano ya mbio za nyika kwa mwaka huu nchini Kenya yatakayofanyika jumamosi ijayo mjini Nairobi.

    Akitangaza timu zitakazoshiriki, makamu wa Rais wa chama cha riadha Kenya Paul Mutwii, amesema kutokana na ongezeko la KWS na NYS mashindano hayo yatajumuisha timu 18 ikiwa ni ongezeko kubwa.

    Katika hatua nyingine makamu huyo wa Rais wa riadha Kenya, amesema timu maarufu za Polisi, Magereza na Jeshi la ulinzi zitaruhusiwa kupeleka timu za vijana chini ya umri wa miaka 20.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako