• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yapanga kutumia miaka mitatu kuboresha mazingira ya vijijini

  (GMT+08:00) 2018-02-06 17:33:52

  Waraka uliotolewa jana na Baraza la serikali la China kuhusu maendeleo ya vijijini umeweka lengo la kuboresha kidhahiri mazingira ya makazi vijijini na kuongeza mwamko wa wanavijiji kuhusu mazingira na afya ifikapo mwaka 2020.

  Waraka huu uliotolewa kwa pamoja na ofisi kuu ya Kamati Kuu ya Chama Cha Kikomunisti cha China CPC na ofisi kuu ya Baraza la serikali la China umefuatilia kuboresha mazingira ya makazi kwenye maeneo ya vijijini nchini China. Ingawa katika miaka ya hivi karibuni maendeleo kadha wa kadha yamepatikana katika kuboresha mazingira ya vijijini, lakini hali ya jumla bado inakosa uwiano, na suala la kutokuwa na usafi na mpangilio bado linajitokeza kwenye baadhi ya maeneo. Waraka huo mpya ndio unalenga kuhamasisha rasilimali na kuimarisha kanuni, kwa ajili ya kusukuma mbele hatua kwa hatua usimamizi wa mazingira ya vijijini.

  Masuala matatu yanayohitaji zaidi udhibiti yaliyotajwa kwenye waraka huo ni takataka za vijijini, kushughulikia maji taka na kuboresha mazingira ya vijijini. Mtafiti wa Taasisi ya sayansi za kijamii ya China Bw. Li Guoxiang amesema, maeneo hayo matatu yanajitokeza sana kwenye maeneo ya vijijini.

  "Takataka za vijijini, asilimia kubwa ni zile ambazo hazijashughulikiwa, au hazikushughulikiwa kikamilifu, kwa hivyo namna ya kushughulikia vizuri takataka hizo, ni kipaumbele kimoja kwenye usimamizi wa mazingira vijijini. Udhibiti wa maji taka vijijini, haswa maji taka kutoka majumbani, bado haujakuwa na utaratibu kwenye maeneo mengi. Tunapaswa kuboresha hatua kwa hatua mazingira ya vijijini kwa kupitia kuweka mpangilio mzuri, kuelekeza ujenzi wa miundombinu na kupitia uungaji mkono wa serikali, ambalo pia ni jukumu moja muhimu."

  China ina eneo kubwa, na zipo tofauti kubwa kati ya sehemu mbalimbali. Waraka huo pia umeweka ratiba tofauti kwa maeneo tofauti. Kwa sehemu za kati na magharibi mwa China zilizoko nyuma kidogo kimaendeleo ikilinganishwa na sehemu za mashariki, lengo ni kuhakikisha asilimia 90 ya takataka za vijijini zinashughulikiwa, na asilimia 85 ya maeneo ya vijijini yana vyoo ifikapo mwaka 2020.

  Mtafiti Li Guoxiang pia amependekeza serikali kuongeza uungaji mkono kwa sehemu za kati na magharibi kwenye usimamizi wa mazingira ya vijijini. Anasema,

  "Udhibiti wa mazingira ya vijijini, unapaswa kuchukuliwa kuwa ni jukumu la serikali, na haupaswi kuwategemea wakulima peke yao. Haswa serikali kuu inapaswa kuongeza uungaji mkono kwa sehemu za kati na magharibi. Kwa namna hii tu, lengo letu la kutimiza usawa wa huduma za umma za kimsingi kote nchini litaweza kufikiwa."

  Waraka huo pia umetaja kuwa serikali kuu itaongeza uwekezaji na kuhamasisha mashiriki mbalimbali ya kijamii kushiriki kwenye miraidi ya usimamizi wa mazingira ya makazi kwenye maeneo ya vijijini kote nchini China.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako