• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Idadi ya watalii nchini China katika msimu wa sikukuu ya mwaka mpya wa jadi kufikia milioni 385

    (GMT+08:00) 2018-02-06 18:15:08

    Naibu mkurugenzi wa idara ya utalii ya China Bw. Wang Xiaofeng leo hapa Beijing amesema kuwa, katika msimu wa sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa China, idadi ya watalii nchini China inakadiriwa kufikia milioni 385, ikiwa ni ongezeko la asilimia 12 ikilinganishwa na mwaka jana kipindi kama hicho, na mapato ya utalii nchini yanatarajiwa kufikia yuan bilioni 476, ambalo ni ongezeko la asilimia 12.5

    Bw. Wang Xiaofeng ameongeza kuwa, utalii umekuwa mtindo muhimu wa watu wa china kusherehekea sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa China, hivyo soko la utalii la China katika msimu wa sikukuu hiyo mwaka huu litaendelea kupamba moto.

    Kwa mujibu wa takwimu, asilimia 83 ya watu wa China wana nia ya kwenda kutalii katika miezi mitatu ya kwanza ya mwaka huu, ambao nusu kati yao wana mpango wa kusafiri katika msimu wa sikukuu ya mwaka mpya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako