• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yaunga mkono kuanzishwa utaratibu mpya wa kuchunguza matumizi ya silaha za kikemikali Syria

  (GMT+08:00) 2018-02-06 18:39:15

  Naibu balozi wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Bw. Wu Haitao amesema ni muhimu kuanzisha utaratibu mpya wa kuchunguza matumizi ya silaha za kikemikali nchini Syria, ili kujua ukweli wa tukio hilo na kuepusha tukio kama hilo lisitokee tena, na kwamba pande zote za baraza la usalama zinapaswa kufanya jitihada za pamoja.

  Balozi Wu Haitao amesema hayo jana kwenye mkutano wa wazi wa Baraza la usalama la Umoja wa mataifa kuhusu suala la silaha za kikemikali nchini Syria. Amesema China inaunga mkono maendeleo katika kazi za kukagua na kuteketeza vifaa viwili vya silaha za kikemikali nchini Syria, na kusisitiza kuwa China inaunga mkono shirika linalopiga marufuku silaha za kikemikali OPCW kuendelea kufanya uratibu na ushirikiano na serikali ya Syria.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako