• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Burundi: Burundi tayari kuandaa COMESA

    (GMT+08:00) 2018-02-06 18:43:07

    Katibu mkuu wa soko la pamoja la kanda ya Mashariki na kusini mwa Afrika COMESA Sindiso Ngwenya amethibitisha kwamba Burundi iko tayari kuandaa mkutano mkuu wa 20 wa soko hilo.

    Kulingana na taarifa kwa vyombo vya habari, Ngwenya amezuru Burundi kutathmini matayarisho ya mkutano huo wa Aaprli 18.

    Kwenye mkutano wa 17 ulioandaliwa, DRC mwaka wa 2014, nchi wanachama walikubaliana kwamba ni zamu ya Burundi mwaka huu ya kuandaa mkutano huo.

    Ngwenya amesema ameridhika na matayarisho yanayoendelea na kwamba walikubaliana na serikali kuandaa hoteli na miundo mbinu mingine husika ili kufanikisha mkutani huo.

    wakati huo huo Ngwenya alisema kuwa Tunisia itajiunga rasmi na COMESA huku nayo Somalia ikijiunga upya na kufikisha idadi ya wanachama kuwa 21.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako