• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Tanzania yaatarajia kuongeza mauzo yake ya mchele Kenya na Rwanda

    (GMT+08:00) 2018-02-06 18:44:44

    Tanzania inatarajia kuongeza mauzo yake ya mchele kwenye masoko ya Kenya na Rwanda kwa thuluthi moja mwaka huu.

    Kulingana na shirika la biashara ya mipakani la Afrika Mashariki, ongezeko hilo litachangiwa na mavuno mazuri ya mwezi Agosti lakini pia bei ya bidhaa hiyo huenda ikapungua kutokana na wingi wake.

    Licha ya kuwepo na mzozo kati ya maswala ya kibiashara ya Kenya na Tanzania, bado Kenya inasalia kuwa soko kuu la mchele wa Tanzania ikifuatiwa na Rwanda.

    Tanzania inatarajia kuuza hadi tani 84,000nchini Kenya na tani 60,000 nchini Rwanda.

    Mauzo nchini Burundi yataendelea kushuka kutokana na mfumko wa bei na kushuka kwa uwezo wa kununua.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako