Imesema kuunganisha mifuko hiyo, hakumaanishi kuwa waliokuwa wafanyakazi katika mifuko hiyo watapoteza ajira zao. Sheria ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii imepitishwa bungeni na hivyo inasubiri saini ya Rais kuwa sheria na kuanza kutumika wakati huo, Serikali ikishughulikia kanuni ikiwemo ya kuweka kikokotoleo cha kiwango cha mafao ya kuliwapa wastaafu.
Akijibu hoja zilizotolewa na wabunge mbalimbali wakati wakichangia Muswada wa kuundwa kwa sheria hiyo bungeni, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, Wenye Ulemavu), Jenista Mhagama alisema wafanyakazi hao wasiwe na wasiwasi kwani ajira zao zipo salama. Hata hivyo alisema, watakaoondolewa ni wasio waadilifu na wasioendana na utendaji wa mfuko.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |