• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya: Watalii waongezeka Kenya

  (GMT+08:00) 2018-02-06 18:46:24

  Idadi ya watalii wa kigeni katika hifadhi za Amboseli na Tsavo nchini Kenya imeongezeka.

  Kulingana na mwenyekiti wa chama cha wenye hoteli tawi la Tsavo na Amboseli Willie Mwadilo, watalii wamekuwa wakiongezeka tangu mwezi Desemba mwaka jana.

  Alisema hoteli kwenye hifadhi hizo zina hadi asilimia 70 na 90 ya wateja ikilinganishwa na kipindi sawa na hiki mwaka jana ambapo kulikuwa na wateja asilimia 30 tu.

  Bwana Mwadilo amesema ongezeko hilo la watalii limechangiwa na kuwepo kwa amani ikilinganishwa na mwaka jana ambapo kulikuwa na uchaguzi na siasa.

  Amesema watalii wengi wanatoka Poland, Italia, Ujerumani na Ufaransa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako