• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda: Mauzo ya bidhaa za kilimo yaongezeka Rwanda

    (GMT+08:00) 2018-02-06 18:47:33

    Rwanda iliuza nje bidhaa za kilimo za thamani ya dola milioni 304 mwaka 2017, hayo ni kulingana na halmashauri ya uuzaji nje wa bidhaa kilimo.

    Mwaka 2016 kipindi sawa na hicho cha kati ya Januari na Septemba Rwanda iliuza bidhaa za dola milioni 232.

    Katika robo ya kwanza ya mwaka 2017/18, mauzo ya bidhaa hizo yaliiletea nchi hiyo zaidi ya dola milioni 116.

    Bidhaa zilizoiletea mapato mengi Rwanda ni kama vile kahawa, chai na pareto.

    Nayo thamani ya mauzo ya matunda ilifikia zaidi ya dola milioni 10 kufikia septemba 2017 ikilinganishwa na dola milioni 5 za kipindi sawa na hicho mwaka 2016.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako