• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Dunia yaendelea kutuma salamu za pole kufuatia kifo cha Shujaa wa Uganda kwenye mchezo wa ngumi, Mzee Peter Sseruwagi

    (GMT+08:00) 2018-02-07 09:07:45

    Wadau wa michezo duniani kote wameendelea kumimina salamu za pole kwa shirikisho la masumbwi kufuatia kifo cha bondia gwiji wa nchi hiyo, Peter Sseruwagi aliyefariki dunia jana kufuatia maradhi ya kisukari aliyokuwa anaugua.

    Sseruwagi anakumbukwa kwa mafanikio makubwa aliyoyapata tangu aanze kushiriki ngumi mwaka 1955, ambapo mwaka 1958 alishiriki kwa mafanikio mashindano ya jumuiya ya madola nchini Uingereza, lakini pia mwaka 1960 alishinda nafasi ya pili kwenye mashindano ya Olimpiki nchini Italia ambako huko mechi zote alizoshinda aliwapiga wapinzani wake kwa knock-out.

    Kisa kingine cha kukumbukwa akiwa bondia ni mwaka 1958 katika mashindano ya kitaifa, pale alipomtwanga kwa knockout bondia kutoka timu ya kuogopwa ya jeshi Idd Amin.

    Akiwa kocha wa timu ya taifa ya Uganda, Sseruwagi alishinda medali ya shaba katika mashindano ya jumuiya ya madola mwaka 1966 nchini Jamaica, na vile vile alishinda medali ya dhahabu nchini Cuba kwenye mashindano ya dunia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako