• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Maendeleo ya ujenzi wa "Ukanda Mmoja Njia Moja" yaimarisha imani ya makampuni ya China kuwekeza nje

  (GMT+08:00) 2018-02-07 16:28:16

  Ripoti ya takwimu kuhusu pendekezo la "Ukanda Mmoja na Njia Moja" kwa mwaka 2017 iliyotolewa na Kituo cha taifa cha Data inaonesha kuwa makampuni yasiyo ya kiserikali yanachukua asilimia 42 miongoni mwa makampuni 50 yenye ushawishi mkubwa zaidi kwenye ujenzi wa "Ukanda Mmoja Njia Moja". Kutokana na ushirikiano wa pendekezo hilo kuendelea kupiga hatua mbele, makampuni yasiyo ya kiserikali ya China yamekuwa na imani zaidi kuwekeza katika nchi za nje.

  Kampuni ya kutengeneza nguo na vitambaa ya Ruyi yenye makao makuu mjini Jining mkoani Shandong ina historia ndefu, na bidhaa zake zimepata umaarufu kwenye masoko ya nchi za Asia Kusini ikiwemo Pakistan na Bangladesh. Baada ya kutolewa kwa pendekezo la Ukanda Mmoja Njia Moja, kampuni ya Ruyi imejenga viwanda vyake katika nchi hizo, ili bidhaa ziweze kutengenezwa katika nchi zinakouzwa. Mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo Bw. Wang Qiang anasema:

  "Tukiangalia hali ya jumla ya sasa, pendekezo la Ukanda Mmoja Njia Moja limeonesha umuhimu mkubwa kwa sekta ya nguo ya China. Tangu pendekezo hili litolewe, kampuni ya Ruyi pia imezindua mkakati wake wa maendeleo katika nchi na sehemu zilizoko kwenye Ukanda huo. Tumeanza na mkoa wa Ningxia hadi mkoa wa Xingjiang, na kwa kufuata mnyororo huu wa uzalishaji na biashara, tukaelekea nchini Pakistan na Bangladesh."

  Wakati makampuni yasiyo ya kiserikali ya China yakishiriki kwenye mchakato wa ujenzi wa Ukanda Mmoja Njia Moja, mbali na kujenga viwanda nje ya nchi, makampuni mengi yalianzisha eneo la ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara katika nchi za nje, na mbinu hiyo pia imepata mafanikio.

  Eneo la viwanda la Rayong nchini Thailand lililojengwa na Kundi la Huali la mkoa wa Zhejiang, China ni mfano wa kuigwa kwenye ujenzi wa Ukanda Mmoja Njia Moja, na pia ni eneo la ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara la ngazi ya kitaifa lililo nje ya nchi. Mpaka sasa eneo hilo lililoanzishwa mwaka 2005 limevutia na kuandikisha makampuni 101 ya sekta mbalimbali kutoka China. Naibu mkurugenzi mkuu wa eneo la Rayong Bw. Wu Guangyun amesema, ujenzi wa eneo hilo umesaidia kuhimiza mafungamano kati ya makampuni ya China katika nchi ya nje.

  "Kwa nini nasema hivyo? Eneo letu limekuwa ni shirikisho la makampuni ya China, na mara kwa mara tunaalika idara za serikali ya Thailand ikiwemo forodha, ushuru na huduma za umeme kuja kwenye eneo letu kushughulikia matakwa ya makampuni yetu, na kufafanua kanuni na sheria husika za Thailand. Aidha, kwa kupitia mawasiliano ya namna hii, makampuni mapya yaliyojiunga na eneo letu yanaweza kujifunza uzoefu wa makampuni yaliyojiunga mapema, na hivyo kusaidia kuhimiza mafungamano na ushirikiano kati yao."

  Uzoefu wa eneo hilo la Rayong umeinua imani ya kampuni za China nchini Thailand. Mwezi Agosti mwaka jana, kundi la Huali lilianzisha eneo lake la pili la viwanda nchini Mexico, ambalo ni la kwanza kuwekezwa na kujengwa na kampuni ya China nchini Mexico na hata katika Amerika kaskazini, na linatarajiwa kuandikisha na kupokea makampuni mwaka huu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako