• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya-NEMA kusubiri kanuni za serikali kuhusu marufuku ya chupa za plastiki

    (GMT+08:00) 2018-02-07 18:35:28

    Mamlaka ya mazingira nchini Kenya,NEMA,imesema haitapiga marufuku matumizi,utengezaji,uuzaji na uagizaji wa chupa za plastiki hadi serikali itakapokuja na muongozo.

    Mamlaka hiyo hapo mwanzo iliwapatia wenye viwanda hadi mwezi Aprili kuanza utekelezaji wa marufuku ya chupa za plastiki.

    Katibu Mkuu wa Mazingira Charles Sunkuli jana alisema kuwa serikali inaandika rasimu ya miongozo kuhusu marufuku hiyo.

    Alisema wizara haijanya mipango yoyote ya kupiga marufuku matumizi ya chupa za plastiki kufikia Aprili na badala yake wanajadiliana na kuandika rasimu ya miongozo ambayo itaeleza ni lini marufuku hiyo itatekelezwa.

    Takwimu kutoka wizara ya mazingiara zinaonyesha kuwa takriban chupa milioni 50 zinatumiwa kwa mwaka nchini kote,ambazo taka zake huharibu mazingira.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako