• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania-TPSF yaomba wawekezaji wa China kuongeza uwekezaji nchini Tanzania

    (GMT+08:00) 2018-02-07 18:35:50

    Taasisi ya sekta binafsi nchini Tanzania (TPSF) imeomba wawekezaji kutoka China kufanya Tanzania nchi ya kipaumbele kwa uwekezaji kutokana na jitihada za Rais John Pombe Magufuli za kuboresha mazingira ya uwekezaji.

    Mwenyekiti wa TPSF Reginald Mengi jana,wakati wa hafla ya chakula cha mchana alichokiandaa baada ya kupokea ugeni wa waziri wa nchi anayeshughulikia masuala ya utawala ,viwanda,na biashara wa China,Zhang Mao.

    Dk Mengi alisema Tanzania ina vivutio vingi kwa wawekezaji wa China wanaotaka kuwekeza nje ya nchi yao.

    Aliwaomba wawekezaji wa China kwenda Tanzania kufanya ubia na wafanyabiashara wa Tanzania ili kuimarisha uhusiano baina ya mataifa hayo mawili.

    Kwa upande wake waziri Mao alihimiza haja ya kuongezwa kwa uwekezaji baina ya mataifa haya na kuwakaribisha wawekezaji wa Tanzania kwenda kuangalia fursa China kwa sababu uchumi wao unakua vizuri.

    Alisema pato la taifa la China lilikuwa kwa asilimia 6.7 kwa mwaka 2017 na kuongeza kuwa wanategemea hali itakuwa nzuri zaidi mwaka huu.

    Aidha Mao alisema China inafanya mageuzi makubwa ya kiuchumi na hasa kutoa fursa ya uanzishaji wa vitega uchumi vya watu binafsi kwa malengo ya kutoa ajira kwa watu milioni 13 kila mwaka.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako