• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya-Wadau wafurahia matokeo mazuri katika sekta ya utalii

    (GMT+08:00) 2018-02-07 18:36:09

    Wadau katika sekta ya utalii nchini Kenya wamesifu ripoti ya hivi majuzi iliyoweka utalii wa Kenya katika mstari wa mbele kimataifa.

    Kwa mujibu wa ripoti ya Travellers Choice iliyotolewa wiki iliyopita,hoteli ya Fairmont Mara Safari Club na Hemmingways Nairobi ziliorodheshwa katika nafasi ya 11 na 22mtawalia,miongoni mwa hoteli 25 bora zaidi Afrika.

    Aidha jiji la Nairobi liliorodheshwa katika nafasi ya tatu kati ya kumi bora za kitalii ulimwenguni.Mkurugenzi Mtendaji wa hoteli za Hemmingways Ross Evans alisema matokeo hayo yatapiga jeki sekta ya utalii nchini Kenya.

    Alitoa wito kwa wadau kutumia matokeo hayo kuimarisha uwekezaji katika sekta hiyo na kuzidisha matangazo kuhusu maeneo ya utalii Kenya kwa mataifa mengine ulimwenguni.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako