• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Uganda-Mfumo mpya wa malipo ya kielektroniki kurahisisha ulipaji kodi

  (GMT+08:00) 2018-02-07 18:36:35

  Mfumo mpya wa malipo ya kielektroniki ambao unawawezesha walipa kodi kutumia kadi zao za VISA, Mastercard na MTN mobile money kulipa kodi umezinduliwa nchini Uganda.

  Mamlaka ya Mapato Uganda (URA) kwa ushirikiano na benki ya Stanbic sasa itawezesha wateja wao kutekeleza majukumu yao kwa kuingia katika wavuti wa URA na kufanya malipo baada ya kuingiza maelezo ya kadi zao au akaunti za MTN mobile money.

  Kulingana na URA,mfumo huo wa malipo utapunguza muda na malipo mengine yasiyo ya lazima.

  Kaimu Kamishna Mkuu wa URA Patrick Mukiibi wakati wa uzinduzi wa mfumo huo alisema URA inajitahidi kuweka mifumo inayoendana na teknolojia ili kupunguza muda na gharama za kufanya biashara.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako