• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Urefu wa barabara za vijijini nchini China wafikia kilomita milioni 4

    (GMT+08:00) 2018-02-07 18:56:16

    Waziri wa mawasiliano na uchukuzi wa China Bw. Li Xiaopeng leo hapa Beijing amesema kuwa, hivi sasa urefu wa jumla wa barabara za vijijini nchini China umefikia kilomita milioni 396, na zaidi ya asilimia 99 ya vijiji sasa vimeunganishwa na barabara lami.

    Bw. Li Xiaopeng amesema katika miaka mitano iliyopita, barabara zilizojengwa upya vijijini zina urefu wa zaidi ya kilomita milioni 1.27. Katika kipindi kijacho, China itatunga sheria kuhusu barabara za vijijini, kuboresha mpango, kuimarisha mwongozo wa kiufundi, kuanzisha mfumo wa uhakikisho wa kifedha, na kuimarisha zaidi usimamizi wa barabara za vijijini.

    Suala la uchukuzi siku zote limekuwa ni kizuizi kwa maendeleo ya uchumi wa vijijini nchini China, na ujenzi wa barabara kumetoa mchango mkubwa kuwaondoa wakulima kutoka kwenye umaskini. Katika miaka ya hivi karibuni, China imeendelea na jitihada za kujenga, kusimamia, kulinda na kuendesha vizuri barabara za vijijini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako