• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Bingwa wa dunia Justin Gatlin akubali kushiriki mbio za Afrika Kusini

  (GMT+08:00) 2018-02-09 08:59:34

  Bingwa wa dunia katika mbio fupi za mita 100, Justin Gatlin wa Marekani anatarajiwa kushiriki mashindano ya Afrika Kusini mwezi machi mwaka huu, jambo lilielezwa kuwa litaongeza msisimko wa mashindano hayo.

  Gatlin ambaye ametwaa ubingwa wa mbio fupi baada ya kumshinda Usain Bolt wa Jamaica anakuwa bingwa wa kwanza wa kimataifa kukubali kushiriki michuano hiyo ya kila mwaka baada ya miaka 16 tangu Michael Johnson afanye hivyo mara ya mwisho mwaka 2001.

  Katika mbio za Afrika Kusini, Gatlin ataanza rasmi ushiriki wake Machi 8 katika mbio fupi za mita 150 mjini Pretoria.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako