• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Sheria ya usalama wa nyuklia ya China yaanza kutekelezwa mwaka huu

  (GMT+08:00) 2018-02-09 16:21:22

  Sheria ya kwanza ya China kuhusu usalama wa nyuklia imeanza kutekelezwa Januari mosi mwaka huu. Ofisa wa Idara ya usalama wa nyuklia ya China amesema utekelezaji wa sheria hiyo una umhimu mkubwa katika kuhakikisha maendeleo endelevu ya shughuli za nyuklia, kulinda usalama wa taifa na maslahi ya umma, na kusukuma mbele ujenzi wa "Ukanda mMmoja njia Mmoja". Carol Nasoro ana zaidi.

  China ikiwa ni moja ya nchi zinazoongoza duniani katika matumizi ya nishati ya nyuklia, idadi na uwezo wa jumla wa mitambo yake ya kuzalisha umeme inachukua nafasi ya tatu duniani, hali inayoifanya kuwa China iwe na jukumu kubwa la kuhakikisha usalama wa nyuklia. Kwa hivyo, sheria ya kwanza ya China kuhusu usalama wa nyuklia imeweka bayana kanuni ya kimsingi ya "usalama kwanza". Mkurugenzi wa kitengo cha usimamizi wa vifaa vya kinyuklia cha Idara ya usalama wa nyuklia ya taifa Bw. Guo Chengzhan anasemaona, kuimarisha kwa hatua kali usimamizi wa usalama wa nyuklia ni umaalumu wa sheria hiyo. Anasema,

  "Sheria hii inaelekeza meagiza kuwa kwa kupitia kuweka vigezo vikali, kuanzisha mfumo kamili, kuimarisha usimamizi na kutoa adhabu kali, mamlaka husika zinatakiwa kufanya usimamizi wa pande zote na kwa wakati wote na kuimarisha udhibiti wa hatari kwa hatua zote zinazohusiana na nishati ya nyuklia, kuanzia usanifu, ujenzi, uendeshaji, na hadi ustaafishaji wa vifaa vya nyuklia, na piahadi jinsi ya kushughulikiaji wa malighafi na takataka za kinyuklia."

  Mbali na hayo, fidia ya hasara za kinyuklia ni kanuni nyingine ya sheria hiyo inayofuatiliwa sana. Sheria hiyo imeweka mfumo wa kulipa fidia ya hasarasa za kinyuklia, na kubainisha kuwa kama ajali ya kinyuklia ikitokea, shirika linaloendesha vifaa vya kinyuklia ni chombo pekee kitakachowajibishwa. Bw. Guo Chengzhan anasema,

  "Sheria ya usalama wa nyuklia ina vifungu 94, na 17 kati yao vinahusu wajibu wa kisheria, na kikomo cha faini kinaweza kufikia yuan milioni tano, na pia inaweza kuagiza kusitishwa kwa ujenzi au uzalishaji, kutoa adhabu za njia mbili kwa wahusika, na kuchukua msimamo wa wazi wa kutovumilia hata kidogo vitendo vya kukiuka sheria."

  Aidha, Sheria hiyo pia inahakikisha uhuru wa umma wa kupata taarifa, na kuweka bayana kuwa idara husika za Baraza la serikali la China, serikali za mitaa na mashirika yanayoendesha vifaa vya kinyuklia wazina wajibu wa kutoa taarifa kwa umma, kukusanya maoni ya umma wakati wa kufanya maamuzi muhimu, na kuitikia ufuatiliaji wa umma, ili kuhakikisha kihalisi maslahi ya wananchi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako