• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya:Kenya kuondoa ushuru wa sekta ya viwanda

    (GMT+08:00) 2018-02-09 17:37:29

    Wizara ya fedha pamoja na viwanda zimeanda majadiliano ya kuondoa ushuru wa baadhi ya bidhaa ghafi zinaozoingia nchini kutoka nje ili kusaidia ukuwaji wa viwanda vya ndani ya nchi .

    Waziri wa viwanda Adan Mohammed amesema mpango huo unalenga kutafuta suluhisho la kudumu la kuwezesha viwanda kupata raslimali kwa bei rahisi.

    Wafanyibiashara watakaoagizia bidhaa za kuendesha viwanda vyao sasa hawatatozwa ushuru.

    Aidha bidhaa zitakazokuja nchini ambazo tayari zimekamilishwa zitakuwa ghali hivyo itaruhusu Kenya kuagiza bidhaa ghafi kwa ajili ya kuvitengeneza Kenya.

    Sekta hiyo inatarajiwa kuongeza pato la taifa kwa asilimia 15 kutoka asilimia 9.2 mwaka 2016.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako