• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya:Kenya kuuza mafuta yake baada ya miaka 4

  (GMT+08:00) 2018-02-09 17:37:54

  Mafuta ya Kenya yataanza kuuzwa katika mda wa miaka 4 ijayo.

  Baada ya kukamilisha utaratibu wa uchimbaji wa mafuta katika visima vilivyosalia,kampuni Tullow Oil imearifu kutumia bilioni 293 katika kumaliza uchimbaji.

  Mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo Mark MacFarne amebainisha kwamba Kenya itaanza kuuza viwango vidogo vya mafuta mwaka ujao.

  Mauzo ya kimataifa ya mafuta hayo yanatarajiwa kuipatia Kenya mapato yatakayoimarisha uchumi kwa kiasi kikubwa.

  Kenya inatarajia kupata faida ya dola 34 kwa pipa na kupunguza gharama ya kununua pipa kwa dola 66.

  Mafuta ya kwanza yatasafirishwa hadi Mombasa kutoka Turkana kwa malori .

  Mauzo ya nje ya mafuta ya kwanza yatafanyika mwaka 2021.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako