• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Uchumi wa Kenya kukua kwa asilimia 5.5

  (GMT+08:00) 2018-02-09 19:09:30

  Takwimu za Benki Kuu ya Kenya (CBK) zinaonyesha kuwa uchumi wa kitaifa utapanuka kwa kiwango cha hadi asilimia 5.5 katika mwaka wa kifedha unaoisha Juni 2018.

  Takwimu hizo zinasema kuwa upanuzi huo wa takribani pointi tatu kutoka kiwango cha sasa cha asilimia 5.2 bado si cha kuridhisha.

  Kwa mujibu wa ripoti ya makadirio ya kiuchumi hali hiyo ilifuatana kwa karibu na msimu mwingine wa kiangazi ambapo bidhaa muhimu ziliadimika.

  Katika utangulizi wa ripoti hiyo, Gavana wa CBK, Dkt Patrick Njoroge amesema kuwa mikakati ya dharura ambayo imewekwa inalenga kuleta manufaa ya kuupa uchumi uhai. Mikakati hiyo ni pamoja na ile ya kuthibiti mfumko wa bei kwa bidhaa muhimu, kuhakikisha kuwa hifadhi ya pesa za kigeni iko thabiti na kutekeleza mikakati ya kupunguza matumizi ya kiserikali.

  Anasema kuwa sekta muhimu kama ile ya Kilimo, utalii na Ujenzi zinaonyesha uthabiti wa kustahimili mipigo ya kukwama na zitabeba uchumi kwa kiwango cha kuupa upanuzi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako